0
Ligi kuu Soka Tanzana Bara Msimu wa
mwaka 2016/17 inafikia tamati
Jumamosi ya Mei 20 ambapo jumla
ya michezo nane itafanyika katika
viwanja mbalimbali nchini.
Jijini Mwanza Mbao Fc watawaalika
Yanga SC katika mchezo ambao
utafanyika kwenye uwanja wa CCM
Kirumba.
Mchezo huu utakuwa miongoni mwa
mechi ambazo zitakuwa na umuhimu
.
Mbao na Yanga
Yanga SC tayari wameonekana
kutetea ubingwa wa Ligi hiyo akiwa
anaongoza msimamo akiwa na alama
68 wakati Simba akiwa katika nafasi
ya pili akiwa na alama 65 wote
wakiwa wamebakiwa na mchezo
mmoja.
Yanga wanahitaji kufunga mchezo huo
ili kuweka heshima ya kumaliza na
pointi nyingi pamoja na kuwa
wachezaji Simon Msuva,Obrey chirwa
watakuwa wakitafuta kiatu cha
dhahabu wakati Mbao Fc ambao wako
katika nafasi ya wakitafuta ushindi kwa
kila njia ili kubaki ligi kuu msimu
ujao.
Simba na Mwadui
Simba atahitaji kushinda mchezo huu
kwa zaidi ya mabao 13 wakati
akiomba Mbao amfunge Yanga kwa
zaidi ya mabao 5 ili kuongeza
uwezekano wake wa kutwaa
ubingwa,Mwadui ambao wako katika
nafasi ya 8 wakiwa na alama 35 hana
la kupoteza katika mchezo huo ambao
utafanyika kwenye uwanja wa Taifa
,Dar Es Salaam.
Azam na Kagera
Ni mchezo ambao utavuta hisia za
wengi kwani nafasi ya tatu imekuwa
na upinzani mkali mshindi katika
mchezo huu atafanikiwa kumaliza
akiwa katika nafasi ya tatu bora.
Azam wako katika nafasi ya tatu
wakiwa na alama 52 wakati Kagera
Sugar wako katika nafasi ya nne
wakiwa na alama 50.
Jkt Ruvu na ndanda
Ndanda Fc ambayo imekuwa
ikikabiliwa na ukata msimu huu baada
ya kuondokewa na wadhamini wake
itakuwa na kazi ya ziada ili kuwafunga
JKT Ruvu ambao licha ya kushuka
daraja wameapa kushuka na ndanda
Fc,mchezo huo ambao utafanyika
katika uwanja wa Nangwada Sijaona
utakuwa mgumu kwa ‘Wanakuchelle’
hao wa kutoka mkoani Mtwara ambao
wanahitaji ushindi ili kubaki Ligi Kuu
msimu ujao.
Ndanda Fc ako katika nafasi ya 14
wakiwa na alama 30 wakati JKT Ruvu
wanavuta mkia wa Ligi hiyo wakiwa
na alama 23.
Stand United na Ruvu Shooting
Mchezo huu pia utakuwa wa hisia
kwani utakuwa kama wa Ruvu
Shooting kulipiza kisasi dhidi ya
Stand United ambao waliwashusha
daraja msimu wa mwaka 2015/16.
Stand United ambaao awali walisema
ukata kuwanyima kumaliza katika
nafasi nne za juu wako katika nafasi
ya 7 wakiwa na alama 35
wakati Ruvu shooting wakishika
nafasi ya 6 wakiwa na alama 36.
Mchezo huu utafanyika kwenye
uwanja wa CCM
Kambarage,Shinyanga.
Majimaji na Mbeya City
Ni mchezo ambao utakuwa na
upinzani mkali kwani timu zote kufikia
sasa haziko salama na kubaki kwao
ligi Kuu msimu ujao utategemea
matokeo ya timu ambazo ziko hatarini
ya kushuka daraja.
Majimaji ambaye ako katika nafasi ya
11 wakiwa na alama 32 watahitaji
alama zaidi ili kuepukana na shoka
hilo wakatia Mbeya City wanashika
nafasi ya 10 wakiwa na alama 33 .
Majimaji anaingia mchezo huo wakiwa
na nguvu mpya baada ya ushindi
dhidi ya JKT Ruvu kuwaongeza
matumaini wakati Mbeya City
walipoteza dhidi ya Yanga kwa 2-1.
Tanzania Prisons na Africa Lyon
‘Wajelajela’ wa kutoka Jijini Mbeya
Tanzania Prisons wanahitaji
kusutumia uwanja wao wa nyumbani
vizuri ili kupata alama tatu za
kuwahaikikishia uwepo wao Ligi Kuu
msimu ujao.
Kufikia sasa Tanzania Prisons wako
katika nafasi ya 9 wakiwa na alama 34
wakati African Lyon wakishika nafasi
ya 13 wakiwa alama 31 timu zote
zinahitaji kushinda .
Mtibwa Sugar na Toto Africans
Mashabiki wa Mwanza watakuwa
wakiufuatilia kwa kina mchezo huu
ambapoa ushindi wa Toto Africans
dhidi ya wenyeji Mtibwa
utawahakikishia nafasi ya kubaki Ligi
Kuu msimu ujao.
Toto Africans ambao wako katika
nafasi ya 15 wakiwa na alama 29
wanahitaji ushindi wa leo wana faida
moja ambayo wanaweza wakaitumia
ya kushambulia kwa mapema na
kupata magoli ya mapema kwa kuwa
Mtibwa Sugar hawana cha kupoteza
katika mchezo huo ambao utafanyika
kwenye uwanja wa Manungu Complex.
Michezo yote itaanza saa kumi kamili
jioni.

Chapisha Maoni

 
Top