'DOREFA' kwa kushirikiana na
Shirikisho la Soka nchini 'TFF'
Wametangaza bei za Viingilio
zitakazotumika katika mchezo wa
Fainali ya Kombe la Shirikisho.
Akivitaja viingilio hivyo Mwenyekiti wa
DOREFA Mulamu Nghambi amesema
kutakuwa na Aina tatu za viingilio
katika mchezo huo utakaopigwa katika
uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
-Kiingilio cha mchezo huo kwa VIP A
kitakuwa Shilingi 20,000 wakati VIP B
kikitarajiwa kuwa Shilingi 15,000 na
jukwaa la mzunguko itakuwa Sh5000,
tiketi tunatarajia zitaanza kuuzwa
Ijumaa Mei 26 mjini Dodoma"
Alisema.
Kuweka oda.
Aidha Nghambi amesema kwamba
kutakuwa na utaratibu wa kipekee wa
kutuma maombi kwa wale watakao
kuwa mbali ili kupunguza msululu wa
watu siku ya Mchezo.
-Mashindano kama ya Kombe la
Dunia Kumekuwa na utaratibu wa
kuweka oda na kulipia tiketi yako
Mapema Lakini hapa utaratibu huo ni
mgumu tutakachofanya ni Makundi ya
watu kuweka oda yako Idadi ya tiketi
wanazotaka ili sisi tuwaunzie na
wakifika tunawapatia, nia ni Kukwepa
usumbufu na misululu ya watu"
Nghambi Alifafanua.
Jumamosi ijao Ya Mei 28 Kiboko Ya
Vigogo nchini Mbao Fc wataumana na
Mnyama Simba SC katika mchezo wa
Fainali wa kombe Azam Sports
Federation, ambapo Bingwa
ataliwakilisha Taifa katika michuano ya
Shirikisho Barani Afrika mwakani.

Chapisha Maoni