0
Timu za Toto Africans na African Lyon
zimeungana na JKT Ruvu kushuka
daraja Msimu huu huku Dar Young
Africans wakitangazwa mabingwa
mara 27 wa Taji la Ligi kuu Soka
Tanzania bara.
Ligi kuu Hiyo ambayo imefikia tamati
Jumamosi ya Mei 20 jumla ya
michezo nane imefanyika katika
viwanja mbalimbali nchini, huku timu
16 zikishuka dimbani kupambana
kuwa katika nafasi nzuri ya msimamo
wa ligi kuu soka Tanzania Bara.
Jijini Mwanza Mbao Fc wamewaalika
Yanga SC katika mchezo ambao
umefanyika kwenye uwanja wa CCM
Kirumba, na kumalizika kwa
mabingwa Yanga kuchapwa kwa bao
1-0, bao pekee la Habib Aji dakika ya
23.
Katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam Simba wameibuka na Ushindi
wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui na
kuwafanya kufikisha alama 68 sawa
na Yanga lakini wakizidiwa idadi ya
Mabao ya kufunga na Kufungwa.
Mabao ya Simba katika mchezo huo
yamefungwa na Shizya Kichuya kwa
njia ya Penati dakika ya 16 huku bao
la pili likifungwa na Ibrahim Ajib
katika dakika ya 25 huku bao pekee la
kufutia machozi la Mwadui likifungwa
na Paul Nonga dakika ya 42.
Azam 0-1 Kagera Sugar.
Katika uwanja wa Azam Complex
Chamazi Jijini Dar es Salaam, Azam
FC wameduwaza na kunyang’anywa
nafasi ya Tatu na Kagera Sugar baada
ya kukubali kichapo cha bao 1-0 bao
ambalo limefungwa na Themi Felix
dakika ya 9.
Toto Africans wameshuka rasmi
daraja baada ya kukubali kichapo cha
mabao 3-1 kutoka kwa wakata miwa
wa Manungu Turiani Mjini Morogoro,
licha ya Toto Africans kuwa wakwanza
kupata bao katika dakika ya 9 ya
mchezo huo kupitia kwa Waziri
Junior.
Tanzania Prisons 0-0 African Lyon
Aidha kwenye uwanja wa
kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya
African Lyon wameungana na Toto
Africans na JKT Ruvu kucheza ligi
daraja la kwanza msimu ujao baada
ya kukubali sare ya bila kufungana.
Mchezo mwingine katika siku hii ya
mwisho ya ligi kuu bara,
iliwakutanisha Wanalizombe Majimaji
na Mbeya City na mchezo huo
umemamlizika kwa Majimaji kuibuka
na ushindi wa mabao 2-1, mchezo
ambao umefanyika kwenye uwanja
Michezo Majimaji Mjini Songea.
Ndanda 2-0 JKT Ruvu.
Wanakuchele Ndanda FC wakiwa
katika uwanja wao wa nyumbani wa
Nangwanda Sijaona wamewaalika
maafande wa JKT Ruvu na
kushuhudia mchezo huo ukimalizika
kwa Ndanda FC kuibuka na ushindi wa
mabao 2-0.
Wapiga debe Stand United
wamewapigisha kwata Wafunga Buti
wa kutoka Mlandizi Mkoani Pwani
Ruvu Shooting kwa Mabao 2-1 katika
mchezo mkali uliofanyika kwenye
uwanja wa CCM Kambarage Mjini
Shinyanga, Bao pekee la Ruvu
Shooting limefungwa na
Abdularhaman Musa ambaye
amefikisha mabao 14 sawa na Simon
Msuva, katika mbio za kuwania tuzo
ya Mfungaji Bora.

Chapisha Maoni

 
Top