0

Man United imetinga fainali ya Europa League na sasa itacheza na Ajax Amsterdam ya Uholanzi ambayo fainali itachezwa Mei 24, mwaka huu jijini Stockholm nchini
Sweden.
Man United imepata sare ya bao 1-1 dhidi ya Celta Vigo ya Hispania ambayo iliing’oa KRC Genk anayochezea Mtanzania Mbwana
Samatta katika hatua ya robo fainali. Shujaa wa Man United alikuwa Marouane Fellain aliyefunga bao la mapema kwa kichwa kabla ya Celta Vigo kusawazisha bao hilo na kutolewa kwa jumla ya mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza Man U waliibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini.



Chapisha Maoni

 
Top