Katika jitihada za kumzuia Muhispania huyo kutimkia Real Madrid, Manchester United
wanajipanga kumpatia mkataba mpya mnono kipa wao
Imeripotiwa kuwa Manchester United wanajipanga kumpatia mkataba mpya David de Gea katika
jitihada zao kumzuia kwenda Real Madrid.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania alikaribia kutua Bernabeu 2015, lakini nyaraka hazikuwa
zimekamilika siku ya mwisho kabla ya kufungwa dirisha la usajili.
De Gea alisaini mkataba mpya kubaki Old Trafford, lakini bado bado miamba hao wa Ulaya bado waliendelea kumfukuzia.
Kwa mujibu wa Manchester Evening News , Mashetani Wekundu wanaamini kumpatia De Gea
mkataba ulioboreshwa kutamshawishi kubaki Manchester.
Mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid amebakiwa na miaka miwili kwenye mkataba
wake, na kuna kipengele cha kuongeza mkataba kwa mwaka mmoja.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni