Serengeti Boys leo Jumapili inakamilisha michezo ya hatua ya makundi kwa kuchuana na Niger.
Maombi ya Watanzania yanatakiwa kuiombea timu hiyo ipate sare au ushindi ili iweze kufuzu hatua
ya nusu fainali. Upande mwingine, ushindi wowote Serengeti Boys
au sare itakuwa imejihakikishia kushiriki fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kufanyika nchini India Oktoba mwaka huu.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 2:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Serengeti Boys inashika nafasi ya pili kwenye kundi B ikiwa na pointi 4 baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Mali na mchezo uliofuata ikaifunga
Angola kwa mabao 2-1.

Chapisha Maoni