0
Nahodha wa Timu ya Mbao FC
Yusuph Ndikumana Raia wa Burundi
amechaguliwa kuwa miongoni mwa
wachezaji watatu watakaowania Tuzo
ya Mchezaji Bora wa Kigeni katika
msimu uliomaliza wa ligi kuu soka
Tanzania Bara.
Ndikumana amepambanishwa na
Kiungo wa Yanga na timu ya Taifa ya
Rwanda Haruna Niyonzima ambaye
anaichezea Yanga Pamoja na Method
Mwanjale raia wa Zimbabwe
anayeichezea Timu ya Simba.
Aidha Timu ya Mbao FC imepata
neema Nyingine baada ya Kocha wao
Mkuu Ettiene Ndairagije kuchaguliwa
kuwania Tuzo ya Kocha Bora wa
msimu ikiwa ni msimu wake kwanza
kufundisha Timu za Tanzania.
Ndairagije ambaye amewahi kuichezea
Timu ya Yanga mwanzoni mwa Miaka
ya 2000 pamoja na kuipatia Ubingwa
wa ligi ya Burundi timu ya Vila’O
Mwaka jana amepambanishwa na
Mecky Mexime mwa Kagera Sugar na
Joseph Omog wa Simba.
Kipa Bora.
Katika kipengele cha Kipa bora wa
Msimu wa mwaka 2016/17, mlinda
Mlango wa Mbeya City Owen Chaima
amechaguliwa kuwania tuzo hiyo
pamoja na Juma Kaseja wa Kagera
Sugar na Aishi Manula wa Azam FC.
Mbaraka Abeid ambaye amemaliza ligi
akiwa na Mabao 12 akiichezea Kagera
Sugar, amechaguliwa kuwania Tuzo ya
Mhcezaji anayechipukia akiwa pamoja
na Mshambuliaji hatari wa Azam FC
Shaaban Idd pamoja na Mohamed Issa
wa Mtibwa Sugar.
Kwa upande wa Tuzo ya mchezaji wa
chini ya umri wa miaka 20 (Tuzo ya
Ismail Khalfan), walioingia katika
kinyang’anyiro hicho ni pamoja na
Shaaban Idd na Abdalah Masoud wote
wa Azam FC pamoja na Mosses
Kitambi wa Simba.
Mwamuzi Bora.
Shirikisho la Soka nchini TFF,
haliwakuaacha waamuzi katika Tuzo
hizo ambapo mwamuzi Shomari Lawi
kutoka Kigoma amepangwa kuwania
Tuzo hiyo pamoja na Elly Sasii wa Dar
es Salaam na Hance Mabena wa
Tanga.
Majina ya mchezaji bora Msimu
yalitolewa Jumatano iliyopita na
upigaji kura unaendelea ukiwahusisha
Makocha wa timu za Ligi Kuu na
Makocha Wasaidizi,Wahariri wa habari
za michezo na Manahodha wa timu
za Ligi Kuu, ambapo mwisho wa
kufanya hivyo ni Jumanne Mei 23
mwaka huu, majina hayo ni Haruna
Niyonzima, Shizya Kichuya, Mohamed
Hussein, Aishi Manula na Simon
Msuva.
Ikumbukwe kwamba sherehe za Tuzo
ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) inatarajiwa kufanyika
Mei 24 mwaka huu ukumbi wa
Mlimani City Dar es Salaam ambapo
Kamati Maalum iliyoundwa kusimamia
tuzo hiyo imefanya mabadiliko kiasi
kwa kuongeza baadhi ya tuzo ambazo
hazikuwepo msimu uliopita lengo
ikiwa ni kuboresha tuzo.
Tuzo zilizoongezwa.
Tuzo zilizoongezwa ni: Tuzo ya
Heshima (ambayo itatolewa kwa
mwanasoka nguli wa zamani mwenye
historia nzuri kwa soka la Tanzania).
Nyingine ni: Tuzo ya Kikosi Bora cha
Msimu (Itatolewa kwa wachezaji Bora
11 wa Ligi Kuu (VPL XI 2016/2017)
walioteuliwa kutokana na ufanisi wao
katika ligi hiyo msimu huu.
Pia imeongezwa Tuzo ya Mchezaji
Bora mwenye chini ya umri wa miaka
20 (Hii itatolewa kwa wachezaji
waliofanya vizuri katika ligi ya vijana
ya timu za Ligi Kuu ya Vodacom.

Chapisha Maoni

 
Top