0

Mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial anataka kuondoka Old Trafford msimu huu wa majira ya joto kwa mujibu wa habari
Anthony Martial anajipanga kumtaarifu Jose Mourinho kwamba anataka kuondoka Manchester United majira ya joto kwa mujibu wa habari.
Chanzo cha Gambling Times kimeripoti kuwa Martial hakuwa na furaha msimu uliopita kwa kukosa nafasi kikosi cha kwanza na anataka kutoka Old Trafford.
Habari hizo zimedai kuwa Martial anataka kumwambia Mourinho kuwa anataka kuondoka Manchester United, ingwa Mashetani Wekundu hao wanataka kumbakisha mchezaji huyo wa Kifaransa, hawatamzuia.
Inaaminika Martial angepende kwenda Paris Saint-Germain majira ya joto, Valencia na RB Leipzig zikitajwa kuwa klabu nyingine zinazotamani kumsajili.
Pia Arsenal, Tottenham na West Ham United ni miongoni mwa klabu za Uingereza ambazo mshambuliaji huyo wa Man United anaweza kutua.
Martial alianza mechi 18 za Ligi Kuu Uingereza msimu uliopita na alikuwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha Jose Mourinho Old Trafford.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alifunga mabao manne na kutoa pasi sita za mwisho katika jumla ya mechi 25 za ligi kwa Mashetani Wekundu waliomaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza lakini wakishinda Kombe la EFL na Europa.


Chapisha Maoni

 
Top