Wagombea wa uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka (TFF), Wallace Karia na Mussa Sima wameshinda mapingamizi yao waliyowekewa na John Kijumbe na Hussen Mwamba.
Kamati ya Uchaguzi wa TFF imetupilia mbali mapingamizi hayo ya wagombea hao waliowekea kwa kukosa sifa ya kugombea nafasi hizo.
Mussa Sima ambaye ni Mwenyekiti wa mkoa wa Singida aliwekea kipingamizi alisema kuwa aliyemuwekea pingamizi hakuna anamfuatilia vizuri kwani yupo kwenye soka zaidi ya miaka mitano.
"Nipo zaidi ya miaka mitano kwenye soka ndio maana nilivyoambiwa nimewekewa kipingamizi kisa udhoefu nilijua nitapita tu katika hilo ma kweli imekuwa hivyo basi nasubili usaili tu ambao unaendelea hivi sasa," alisema Sima.
Wakati huu kinachoendelea hapa makao makuu ya TFF Karume ni usaili wa wagombea na wanakwenda kutokana na aliyewahi kuandika jina kwenye karatasi ya waliofika leo hapa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni