0
KLABU ya Arsenal imeanza mazungumzo na Lyon ya Ufaransa juu ya usajili wa mshambuliaji, Alexandre Lacazette.
Timu kadhaa zimeonyesha nia ya kumsajili Lacazette, lakini inafahamika Arsenal ipo karibu kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekuwa mchezaji namba moja kati ya wanaowaniwa na Arsene Wenger, baada ya mpango wa kumsajili nyota wa Monaco, Kylian Mbappe kupoa.
Mazungumzo kati ya Rais wa Lyon, Jean-Michel Aulas na The Gunners yalifanyika wiki hii na yataendelea wiki ijayo katika harakati za Wenger kujaribu kukamilisha usajili wa mchezaji huyo kabla ya kuanza maandalizi ya msimu mpya.
Arsenal ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Lyon juu ya kumsajili mshambuliaji, Alexandre Lacazette PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Lacazette amefunga mabao 37 katika mechi 45 za Lyon msimu uliopita, yakiwemo 28 ya Ligue 1 na alitarajiwa kuhamia Atletico Madrid kabla klabu hiyo ya Hispania haijafungiwa kusajili.
Tayari mchezaji huyo aliyezaliwa miaka 26 iliyopita amethibitisha nia yake ya kuhama na amesema Arsenal kupoteza makali kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya hakuwezi kuwa sababu ya kumzuia kuhamia Emirates.
Lyon inaweza kutaka ada ya uhamisho ya zaidi ya Pauni Milioni 35 kutoka Arsenal na Rais wa klabu hiyo, Michel Aulas anaweza kutumia ofa waliyotaka ada ya uhamisho ya rekodi ya dunia waliyotaka kutoa kwa Mbappe kama kigezo cha kuomba kiais hicho.
Mchezaji mwenzake, Mbappe, Thomas Lemar pia anatakiwa na Wenger, lakini haijawa wazi kama Monaco itaruhusu wachezaji zaidi kuondoka, kufuatia kuondoka kwa Bernardo Silva kuwa njiani kuondoka kwa Tiemoue Bakayoko.

Chapisha Maoni

 
Top