Klabu ya Bournmouth imekaribia kumsajili beki wa Chelsea, Nathan Ake kwa dau la Pauni 20 milioni.
Awali, Ake alitolewa kwa mkopo na klabu yake katikati ya msimu wa 2016/17 kwenda Bournmouth kabla ya kurejea Chelsea na kufanikiwa kufunga mabao matatu katika mechi 12 alizocheza huku akiisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa msimu uliopita.
Gazeti la The Sun lilidokeza kwamba awali Bournmouth iliweka mezani Pauni 18 milioni jambo ambalo lilikataliwa.
Imeelezwa kwamba usajili huo utakamilishwa baada ya mchezaji huyo kurudi kutoka mapumzikoni.
Chapisha Maoni