0
Mshambuliaji Shiza Kichuya jana alikuwa nyota wa mchezo baada ya kuifungia Taifa Stars mabao mawili katika mechi ya ufunguzi wa mashindano ya Cosafa dhidi Malawi nchini Afrika Kusini.
Kichuya alifunga mabao hayo katika dakika ya 13 na 18 huku akitunukiwa zawadi ya mchezaji bora wa mechi hiyo iliyomalizika kwa Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Kichuya alifunga bao la kwanza akimalizia krosi ya Saimon Msuva wakati bao lake la pili lilitokana na shuti kali alilopiga, akimalizia pasi ya Elias Maguli.
Baada ya ushindi huo, Stars itakabiliana na Angola katika mchezo unaofuata kwenye Kundi A ambao utafanyika Juni 27.

Chapisha Maoni

 
Top