0
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anataka kusajili mabeki wanne wapya – Dani Alves, 34, kutoka Juventus, Kyle Walker, 27, kutoka Tottenham, Ryan Bertrand, 27, kutoka Southampton na Benjamin Mendy, 22, kutoka Monaco (Star on Sunday).
Wanasheria wa Cristiano Ronaldo wanadai kuwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid, alilipa kodi nyingi kupita kiasi kwa mamlaka za Spain, na sio kidogo kama inavyodaiwa (Cadena Cope).
Manchester United wamempa mkataba wenye thamani ya euro milioni 7.5 kwa msimu, kiungo wa Roma Radja Nainggolan (Il Tempo).
Liverpool wanataka kuongeza kasi zaidi kwa kumtaka Alex Oxlade-Chamberlain wa Arsenal baada ya kukamilisha usajili wa Mohamed Salah (Mirror).
Jose Mourinho ameitaka Manchester United “kuvunja benki” na kutoa pauni milioni 100 ili kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane na kuachana na Cristiano Ronaldo (Sunday Mirror).
Arsenal watamgeukia Anthony Martial wa Manchester United iwapo watashindwa kumsajili Kylian Mbappe kutoka Monaco (Mail Online).
West Ham wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 25 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott (Daily Mirror).
Liverpool hawataki kukata tamaa ya kumsajili Virgil van Dijk na wameambiwa na Southampton kuwa beki huyo atagharimu pauni milioni 70 (The Express).
Real Madrid wamebadili mawazo yao ya kutaka kumchukua Zlatan Ibrahimovic kwa mkataba wa muda mfupi (Don Balon).
Chelsea wapo tayari kuwapa Juventus, Cesar Azpilicueta, kama fedha peke yake hazitatosha ili kumsajili Alex Sandro (Calciomercato).
Rafael Varane ameshawishiwa kubakia Real Madrid, huku kukiwa na taarifa kuwa Manchester United inamnyatia (Marca).
Manchester United wanamtaka beki wa Barcelona Jordi Alba, lakini wamekiri wenyewe kuwa itakuwa vigumu kumpata (The Sun).
Inter Milan wamewaambia Juventus kuwa wanaweza kumsajili, Ivan Perisic, ambaye anasakwa na Manchester United (Tuttosport).
Dani Alves amejaribu kumshawishi Paulo Dybala kwenda naye Manchester City (Corriere dello Sport).
Juventus watamruhusu Alex Sandro kujiunga na Chelsea iwapo mchezaji mwenyewe ataomba kuondoka (Metro).
Kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko anajiandaa kufanya vipimo vya afya Chelsea wiki ijayo (Evening Standard).
Paris Saint-Germain wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 60 kumtaka mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero (The Times).
Chelsea wapo tayari kumruhusu mshambuliaji wake Loic Remy kuondoka kwa bei poa (The Sun).
Ross Barkley anataka kuondoka Everton ili kupata muda zaidi wa kucheza, ili aweze kuingia katika kikosi cha timu ya taifa ya England huku Kombe la Dunia likinukia (Sun).
Rais wa Lyon amesema Arsenal lazima waongeze dau lao na kufikia pauni milioni 57 iwapo wanataka kumsajili Alexandre Lacazette, 26 (L’Equipe).
Arsenal wameanza mazungumzo kuhusu mkataba mpya na kiungo Alex Oxlade-Chamberlain, 23 (Sun).
Kiungo wa zamani wa Tottenham, Paulinho, 28, amesema Barcelona wanataka kumsajili, lakini hana mpango wa kuondoka Guangzhou Evergrande ya China (Globo).
Mshambuliaji wa Arsenal Chris Willock, 19, anakaribia kujiunga na Benfica bila malipo yoyote (Sunday Mirror).
Bournemouth wanajiandaa kumsajili beki wa Chelsea Nathan Ake, 22 kwa pauni milioni 20 (Sun).
Newcastle na Southampton wanataka kumsajili beki wa Arsenal Calum Chambers, 22 (Evening Chronicle).
Valencia wanataka kumsajili kipa wa akiba wa Arsenal Emiliano Martinez, na wapo tayari kutoa pauni milioni 5 (Sun).
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa.

Chapisha Maoni

 
Top