0
Katibu Mkuu wa Dar Young Africans Charles Boniface Mkwasa amewaomba Wanachama, wapenzi na Mshabiki wa Timu ya Yanga kuwa watulivu katika kipindi hiki cha Usajili na Kwamba wanapaswa kusikiliza zaidi taarifa kamili kutoka katika klabu hiyo na Si Stori za vijiweni.
Mkwasa amesema taarifa yoyote inayohusu mchezaji kusajiliwa ama kuachwa itatolewa na Klabu hivyo wanapaswa kuuamini uongozi waliouweka na watafanya kazi nzuri.
-Tunawaomba Sana wapenzi wetu wao makini na Taarifa za Mitandao ya kijamii, Kama klabu bado hatujatangaza nani tumemsajili au Nani tutamuacha na Ningependa Sana watu wawe watulivu na kusubiri Taarifa zetu" Alisema.
Juma Abdul.
Akizungumzia kuhusu taarifa za Kuwazuia Nyota wao kuondoka ndani ya Timu hiyo kama Mlinzi Juma Abdul, Mkwasa amesema wao kama klabu Wanaamini katika Maendeleo ya mchezaji na Kama akipata Timu nzuri hawatakuwa na uwezo wa kumzuia.
-Ifahamike wazi kwamba sisi hatujamzuia mchezaji yeyote Kwani tunaamini katika Maendeleo yao, Ila Kwa kifupi hatuwezi kumruhusu mchezaji wetu Nyota Ahamie moja ya timu za hapa nyumbani Kwani uwezo wao tunaujua" Mkwasa aliongeza.
Usajili wa Mbwembwe.
Ikumbukwe kwamba katika kipindi cha Usajili Yanga Ndio Waliokuwa Tishio kwa kipindi cha nyuma Lakini mpaka sasa Hakuna mchezaji Nyota aliyehamia katika timu hiyo Huku wapinzani wao Simba ambao awali walikuwa watulivu tayari wamekwishawasajili Aishi Manula, Shomari Kapombe kutoka Azam na Nyota wa Mbao FC Jamali Mwambeleko miongoni mwa wengine.

Chapisha Maoni

 
Top