0
Mkurungezi wa ufundi wa Barcelona, Robert Fernandez anaamini hakuna klabu itakayoweza kulipa gharama ya Neymar ya euro 222milioni.
Nyota huyo wa Brazil amesaini mkataba mpya wa miaka mitano mwezi Juni ambao thamani yake imeongezeka kutoka euro 200milioni hadi euro 222milioni na utafikia euro 250milioni utakapofikia miezi 12.
Neymar alikuwa akihusishwa na kutaka kuondoka Camp Nou kabla ya kusaini mpya na kumaliza uwezekano wa kujiunga na Manchester United au Paris Saint-Germain.
Hata hivyo, magazeti yameandika Jumatatu kuwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 25, hana furaha ndani ya Catalonia na anajiandaa kuondoka msimu huu.
Robert, anaamini hakuna klabu yoyote itakayoweza kufikia dau hilo.
Wakati alipouliza itakuwaje Barca bila ya Neymar, alijibu: "Sidhani kama hilo litatokea."
Aliongeza: "Siyo lengo letu kupoteza wachezaji, labda ambao si wakiwango cha juu. Tunajaribu kuboresha kikosi chetu kwa kila namna."

Chapisha Maoni

 
Top