Klabu ya Leicester City imejipanga kumpa mshahara mnono nyota wa Swansea, Gylfi Sigurdsson ambaye anatajwa kukaribia kuhamia Everton msimu huu.
Sigurdsson alifanikiwa kufunga mabao tisa na kutoa basi 13 za mabao kwenye msimu uliopita wa Ligi Kuu England jambo lililofanya timu mbalimbali za England kumtolea macho.
Everton wamekuwa vinara wa kutaka kumsajili mchezaji huyo kwa siku za hivi karibuni kutokana na kuendelea kumfuatilia.
Pia Leicester City imeripotiwa kuwa kwenye rada za kumkamata mchezaji huyo wa zamani Tottenham ambaye kwa sasa anakipiga Swansea kutokana na kuwapoteza wachezaji wengi nyota kwenye kikosi chake waliohamia klabu zingine msimu huu.
Chapisha Maoni