0
Mashabiki wanane wamefariki dunia uwanjani nchini Senegal na wengine 48 kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wakati wakiruka ili kujiokoa kwenye vurugu zilizotokea uwanjani hapo.
Vurugu hizo ziliibuka wakati wa mechi ya fainali Kombe la Ligi iliyozikutanisha klabu za Stade de Mbour na Union Sportive Quakam.
Mapigano yaliibuka uwanjani biana ya mashabiki na polisi na walinda usalama hao walijibu kwa kuwarushia maji ya kuwa pamoja na mabomu ya machozi, jambo lililoongeza ghadhabu kwa mashabiki hao na wengine kujiokoa kwa kuruka ukuta.
Mpaka dakika 90 timu hizo zilifungana mabao 1-1 na katika muda wa nyongeza Mbour walikuwa wa kwanza kupata bao na kufanya matokeo kuwa 2-1, jambo lililosababisja kuibuka vugugu kutokana na wapinzani wao kugomea bao hilo.

Chapisha Maoni

 
Top