Kiungo Nemanja Matic yuko mbioni kuondoka Chelsea baada ya kuachwa katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya kama ilivyokuwa kwa Diego Costa.
Kiungo huyo anayewaniwa na Manchester United na Juventus hakusafiri na timu yake iliyokwenda ziarani China na Singapore.
Kocha Antonio Conte ametoa mwanya kwa kiungo huyo Mserbia kukamilisha masuala yake, wakati mwenzake Costa akiwa bado Brazil wakati akiangalia namna ya kurudi Atletico Madrid.
Matic aliripoti katika mazoezi kama wachezaji wengi wa Blues, lakini muda mwingi alikuwa akifanya mazoezi peke yake.
Kocha wa Man United, Jose Mourinho anahamu ya kutaka kumsajili kiungo huyo wa zamani Benfica, lakini Chelsea wanaonekana hawapo tayari kuwapa wapinzani wao silaha.
Hasa baada ya bosi huyo wa Old Trafford kumpora Romelu Lukaku katika mikono ya Blues, jambo linalotoa uwezako wa nyota huyo kutimikia Juventus.
Kukamilika kwa usajili wa pauni 39.7 milioni wa Tiemoue Bakayoko ni wazi kunafungua mlango kwa Matic kuondoa katika kikosi cha Conte.
Chapisha Maoni