Kocha wa Mbao, Etienne Ndyaragije amesema timu yake haijapungukiwa nguvu kama watu wengi wanavyozani baada ya kuondokewa na nyota wake.
Ndyaragije alisema kikosi chake kilikuwa na nyota takribani thelathini, hivyo kuondoka kwa nyota watano haiwezi kusumbua bali ni kuziba nafasi zao ambazo wameziacha wazi.
"Siyo rahisi kusema kuwa Mbao tumeyumba, ila wameondoka wachezaji ambazo walikuwa katika kiwango kizuri, ila wapo ambao wanaendelea na sisi na wataziba nafasi za wachezaji walioondoka, "alisema.
Tuliendesha majaribio hapa walijitokeza wachezaji wengi sana ambao wanavipaji, na sisi falsafa yetu ni kuinua vijana na kisha kuonekana halafu kuwauza na ndivyo tunavyofanya msimu huu.
"Kuna wachezaji wengi hapa Tanzania kiukweli, yani walikuja vijana wengi katika majaribio na nimewachuja na kupata vijana ambao watakuwa na sisi ila bado hatujamalizana nao nazani wiki ijayo kila kitu kitakaa saws, alisema.
Akizungumzia kuhusishwa na klabu ya Simba alisema kuwa taarifa hizo alikuwa akizisikia hata yeye, lakini alishamalizana na Mbao muda mrefu, kwahiyo ilikuwa ikimshangaza hata yeye mwenyewe kuhusishwa kujiunga na klabu hiyo.
"Nilisikia muda mrefu nahusishwa kwenda huko, lakini mimi nilimalizana muda mrefu na Mbao, na ndio maana leo hii nipo hapa nikifanya kliniki ya wachezaji mimi mwenyewe, ningekuwa sihusiki angekuwepo mwingine, "alisema.
Naye Mratibu wa timu hiyo Masalinda Njashi alisema kuwa timu yao imekuwa ikisajili kwa umakini bila kukurupuka, huku akimsifu kocha wao kwa jinsi ambavyo anasimamia kliniki hiyo.
Chapisha Maoni