0
Kikosi cha Timu ya Simba kimewasili Salama Nchini Afrika Kusini ambapo wanatarajiwa kupiga kambi ya siku 20 kwa ajili ya maandalizi ya Kabla Kuanza kwa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.
Simba ambao waliondoka Jumatatu asubuhi watakuwa Mjini Johannesburg ambapo wakiwa huko wamepangiwa kucheza michezo kadhaa Za kirafiki na timu za Ligi Kuu nchini Humo.
Emmanuel Okwi
Miongoni mwa wachezaji ambao wamesafiri na timu hiyo ni pamoja na Jonas Mkude, James Kotei, Laudit Mavugo pamoja na Kipa Emmanuel Mseja aliyesajiliwa kutoka klabu ya Mbao huku Mshambuliaji Emmanuel Okwi ambaye hakusafiri na timu kwa kukosa Visa kwa wakati akitarajiwa kuungana na timu hiyo Baadaye.
Wachezaji ambao hawakusafiri na Simba
Aidha wachezaji Yassin Mzamiru, Said Ndemla, Kichuya, John Bocco na Kipa Aishi Manula ambao wako na timu ya Taifa, Taifa Stars inayoshiriki michuano ya kufuzu kwa Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani CHAN yatakayofanyika Jijini Nairobi, Kenya wakitarajiwa kuungana na timu Timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa marudiano utakaofanyika Rwanda Julai 23.

Chapisha Maoni

 
Top