Mshambuliaji wa Manchester United, Wyne Rooney wiki hii anatarajiwa kutua kwenye klabu yake ya zamani ya Everton na ataendelea kulipwa mshahara wake wa awali wa Pauni 250,000 kwa wiki.
Manchester United pia imetangaza kutega Pauni 20 milioni kwa ajili ya kudaka saini ya mshambuliaji wa Arsenal, Oliver Giroud.
Rooney mwenye miaka 31 huyupo kwenye kikosi cha Manchester United ambacho kitatua Marekani Jumapili wiki hii ikiwa ni ziara yao kabla ya msimu kuanza.
Taarifa zilizopatikana klabuni hapo jana Jumanne, mipango yote ya uhamisho wa Rooney tayari imekamilika kwa uhamisho wa Pauni 26.5 milioni.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni