Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kuvunjwa Baraza la Michezo la Tanzania (BMT) baada ya kutoridhishwa na utendaji wa wake.
Majaliwa aliagiza leo kuwa, baraza hilo livunjwe na shughuli zake zitafanywa na sekretarieti hadi hapo litakapoundwa tena.
Awali, Waziri Mkuu alimuagiza Waziri mwenye dhamana ya michezo, Dk Harrison Mwakyembe kulifanyia tathmini baraza hilo kuhusu utendaji wake na akiona kuna upungufu alivunje na kisha aliunde upya.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni