0

STRAIKA Pastory Athanas wa Simba ametua rasmi katika klabu ya Singida United na kupewa mkataba wa miaka miwili, baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu iliyokuwa inaendelea kutokana na mchezaji huyo kuwa na mkataba na klabu ya Simba.
Mkurugenzi wa timu hiyo, Festo Sanga alisema usajili wa mchezaji huo wanaimani utaongeza nguvu katika kikosi chao katika mashindano watakayoshiriki kwa msimu ujao.
Sanga aliongeza kuwa mchezaji huyo anaenda kujiunga moja kwa moja na wachezaji wenzake waliopo Dodoma kwa ajili ya kambi ya mkoani Mwanza ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao.


Chapisha Maoni

 
Top