Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania 'Taifa Stars' Salumu Shabani Mayanga amejiwekea Imani kubwa timu yake itaibuka kidedea katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Zambia ya Michuano ya Nchi za Ukanda wa Afrika ya Kusini 'CECAFA'.
Licha ya wachambuzi wengi nchi Afrika Kusini kusema kwamba kiufundi Tanzania wapo vibaya Lakini Mayanga amesisitiza kuwa lazima ataibuka na ushindi katika mchezo huo utakaopigwa Jumatano Ya Julai 5 katika uwanja wa Moruleng.
-Kitu ambacho Kwa sasa tunakihitaji sana ni matokeo mazuri, tumechambwa Sana kwamba Hatuna mchezo mzuri Lakini Tupo kwenye nusu fainali sasa, Nawapongeza wachezaji Wangu kwa kufuata maelekezo yangu na sasa nia yetu ni ushindi dhidi ya Zambia" Mayanga Alisema.
Ameongeza kuwa "Tunawajua waZambia kuwa ni timu nzuri, tumekutana nao Mara kadhaa na wametusumbua, Lakini vijana kwa sasa wanahamu ya kufika fainali, ninaimani kubwa watatimiza hazma yao".
Rekodi.
Mara ya Mwisho Kwa Tanzania na Zambia kukutana katika michuano hiyo ilikuwa ni Julai 5, Mwaka 1997 ambapo timu hizo zilitoka Sare ya 2-2 mabao ya Tanzania yalifungwa na Edibilly Lunyamila na Hussein Marsha Huku Yale ya Zambia yakiwekwa Wavuni na Masauso Tembo na Alex Namazaba.
Kama Mayanga atafanikiwa kushinda katika mchezo huo, atakuwa amejiwekea rekodi ya kipekee ya kutofungwa katika michezo nane mtawaliwa kwenye mashindano mbalimbali.
Nyumbani
»
African Sport
» Kocha mkuu wa timu ya Tanzania Taifa stars aapa kuwashikisha adabu Zambia
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni