0

Timoth Weah ambaye ni mtoto wa mshindi wa Tuzo ya Ballon d’Or amesajiliwa kwenye klabu ya Paris Saint-Germain.
Mchezaji huyo kinda mwenye miaka 17 alitangazwa rasmi jana Jumatatu kuitumikia miamba hiyo ya Ufaransa kwa mkataba utakaoisha mwaka 2020.
Timoth alijiunga na Ligue 1 tangu mwaka 2014 na msimu uliopita alifanikiwa kufunga ‘hat trick’ kwenye timu ya vijana dhidi ya Ludogorets katika mashindano ya vijana ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Baba yake Timoth, ambaye ni raia wa Liberia aliitumikia PSG kati ya mwaka 1992 na 1995 na baadaye akatwaa Tuzo ya Ballon d’Or muda mfupi baada ya kuhamia AC Millan.


Chapisha Maoni

 
Top