Mchezaji anayetajwa kuwakosesha usingizi mabosi wa klabu za Real Madrid na Arsenal, Kylian Mbappe anatarajia kukutana na Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi akiwa na Mkurugenzi wa Michezo, Antero Henrique, huku nyota huyo akisindikizwa na baba yake mzazi ili kuzungumzia uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo.
Mwishoni mwa wiki iliyopita iliripotiwa kwamba Arsenal walitangaza kuweka mezani dau la usajili linalofikia Pauni 125 milioni.
Hata hivyo mabingwa wa soka barani Ulaya, klabu ya Real Madrid imekuwa ikimfuatilia mchezaji huyo kwa ukaribu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni