Tetesi za kuwa kiungo wa Taifa Stars, Mzamiru Yassin amezivutia timu kadhaa nchini Afrika Kusini, zimemfurahisha mchezaji huyo wa Simba.
Mzamiru ni mmoja kati ya wachezaji wanne wa kikosi cha Taifa Stars ambao waling’ara kwa kuwa wachezaji bora wa michezo minne tofauti ambayo timu hiyo imecheza katika michuano ya Cosafa.
“Hizo ni taarifa ambazo nimezisikia lakini bado hakuna timu ambayo imenifauta, lakini ni taarifa njema kama zitakuwa na ukweli ndani yake.
“Hakuna mchezaji ambaye hana utayari wa kupiga hatua, binafsi nimefurahia na ni ndoto yangu kucheza Afrika Kusini, ukisema utaji ligi bora Afrika, huwezi kukosa kuitaja hiyo,” alisema Mzamiru.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni