Yanga imemtambulisha Dismas Ten kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino akichukua nafasi ya Jerry Murro.
Kwa kipindi kirefu mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara walikuwa hawana msemaji kutokana na Murro kufungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Licha ya Murro kutoka kifungoni lakini Yanga imemua kuajiri Ofisa Habari mwingine.
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa alisema Ten anakuwa mkuu wa kitengo cha habari akitokea Mbeya City na wana imani kwa uzoefu wake ataisaidia klabu hiyo katika masuala ya habari na hata kuiingizia kipato.
Naye Ten aliishukuru Yanga kwa kumpatia nafasi hiyo na kuahidi kufanya kazi kwa weledi ili kuiletea maendeleo klabu hiyo.
Ten alisema anashukuru kupata nafasi katika klabu kubwa kama Yanga na anaomba ushirikiano ili ili kuhakikikisha malengo ya klabu yanafikiwa.
Chapisha Maoni