Unamkumbuka yule kiungo wa kati wa timu ya Madini FC “Rasta’ aliyependwa na Simba katika mechi yao ya robo fainali ya Ligi ya FA, hadi Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hans Pope akaonesha nia ya kuhitaji huduma yake, sasa wamemtema rasmi.
Awesu Awesu ‘Rasta’ awali alithibitisha kuwa kwenye mazungumzo na timu ya Simba lakini baadaye Yanga nao walionyesha nia ya kumhitaji mchezaji huyo hivyo wakawa kwenye mazungumzo kwa pamoja.
Awali, mwenyekiti wa usajili wa simba, Hans pope alisema kuwa wamevutiwa na huduma ya Kiungo huyo anaeonekana kuwa na nguvu ya miguu huku akijiamini bila kujali mpinzani anaekutana nae hivyo wanatamani kuwa nae msimu ujao na watatoa taarifa mapema baada ya kukamilikisha mazungumzo.
Hata hivyo dirisha la usajili wakati likielekea ukingoni bado Rasta hajafanikiwa kusikika kwenye orodha ya majina ya klabu za Yanga na Simba ambazo alikuwa nao katika mazungumzo achilia mbali Singida United ambao aliwasiliana nao kwa simu.
Chapisha Maoni