Liverpool imekamilisha usajili wa kiungo Alex Oxlade-Chamberlain kutoka Arsenal kwa dau la paundi milioni 40
Chamberlain mwenye umri wa miaka 24 alikataa kujiunga na Chelsea hapo jana licha ya vilabu hivyo viwili kukubaliana huku akijiunga Liverpool kwa mkataba wa miaka mitano na mshahara wa paundi 120,000 mwa wiki.
Muingereza huyo ambaye alikuwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake alikaa kusaini mkataba mpya wenye thamani ya paundi 180,000 kwa wiki kwenye klabu yake ya Arsenal.
Oxlade-Chamberlain ameichezea Arsenal mechi 198 tangu ajiunge nayo mwaka 2011 akitokea Southampton Agosti 2011 huku akifunga jumla ya magoli 20.
Baada ya kukamilisha usajili huo, Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amefurahishwa na usajili huo huku akidai kuwa hakuhitaji kufikiria mara mbili kumsajili mchezaji huyo.
Kocha huyo amemtaja Chamberlain kama mchezaji mwenye mtazamo chanya ambaye yupo tayari kujitoa mhanga na ana maono ya kufanya vizuri zaidi.
“Huyu ni mtu ambaye amefanya uamuzi mgumu kutoka klabu kubwa na kuja kwenye klabu nyingine kubwa na nafikiri alikuwa na ofa kutoka sehemu nyingine, kwahiyo kumpata ni furaha kubwa”, alisema.
Nyumbani
»
Transfer News
» Liverpool Yamnasa Oxlade-Chamberlain Kutoka Arsenal Kwa Paundi Milioni 40
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni