Timu ya Misosi FC imeibuka mabingwa wapya wa Ndodo Cup 2017 baada ya kuifunga Gomz penalti 5-4.
Mchezo huo wa fainali ulifika hatua ya matuta baada ya kuisha dakika tisini na kutoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo uliofurika mashabiki kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, ilishuhudiwa mashabiki wakishangilia kwa kuingia katikati ya uwanja jambo lililowapa askari kazi ya ziada kuwatimua.
Chapisha Maoni