Klabu ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Mlandege FC ya visiwani Zanzibar.
Katika mchezo huo ambao umepigwa kwenye dimba la Amaan visiwani humo, mabao ya Yanga yaliwekwa kimiani na mshambuliaji mpya wa klabu hiyo aliyetokea Simba, Ibrahim Ajibu pamoja nae Emmanuel Martin
Yanga wamepata ushindi huo ikiwa ni siku moja tu tangu wapokee kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Chamazi ikiwa ni mwendelezo wa mechi za kujipima nguvu kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa Ligi.
Baada ya mchezo huo wa leo, Yanga itaondoka kuelekea visiwani Pemba kwa kambi ya siku 10 kujindaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa jadi, Simba, ambao utapigwa Agosti 23 kwenye uwanja wa taifa mwaka huu.
Kikosi cha Yanga kilichoanza leo dhidi ya Mlandege:
Ramadhani Kabwili (GK), Juma Abdul, Haji Mwinyi, Pato Ngonyani, Nadir Haroub (C), Maka Edward, Yusuph Mhilu, Raphael Daudi, Matheo Anthony, Said Mussa, Baruan Yahya Akilimali.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni