Mabingwa wa Kombe la Azam Sports Federation Simba Sports Club wamefanikiwa kutwaa Ngao ya Hisani baada ya kuibuka na ushindi wa penati 5-4 baada ya Dakika 90 kumalizika Kwa Sare ya 0-0.
Mchezo huo ambao umefanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, ulitawaliwa na utulivu Kwa dakika zote 90 Licha ya mihemuko Ya Kabla ya mchezo huo.
Dakika ya 45.
Mchezo ulianza Kwa Yanga kufanya mashambulizi ya Harakaharaka na kupata Kona Mbili za Mapema Huku Simba ambao wakitulia na kujaribu kupiga Pasi fupufupi.
Katika Kipindi hicho Mwamuzi Heri Sassi alilazimika kuwapa kadi za Njano Nahodha wa Simba SC Method Mwanjali na Mlinzi wa pembeni wa Yanga SC Juma Abdul.
Hadi Kipindi cha pili kilichotawaliwa zaidi na Simba kinamalizika Yanga SC ambao walikuwa Nyumbani Sifuri na Simba Sifuri.
Kipindi cha pili.
Kipindi cha pili kilianza kwa taratibu zaidi na Yanga walionekana kufuta makosa ya kipindi cha pili kwa kumiliki Mpira kwa dakika tano za kwanza.
Dakika ya 53 Mzimbabwe Thabani Kamusoko alipiga Shuti la umbali wa kama mita 30 ambalo lilipaa kidogo juu ya Lango la Simba, Lakini hiyo ilifuatiwa baada ya Haruna Niyonzima kuoneshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Juma Abdul.
Simba Ndio walikuwa wa kwanza kufanya mabadiliko kwa kumtoa Laudit Mavugo na kumuingiza Juma Luizio katika dakika ya 71 na dakika 74 Yanga nao wakamtoa Raphael Daudi na kumuingiza Juma Mahadhi.
Dakika ya 81 Simba walikosa bao la wazi baada ya Kipa Rostand Youthe kukosa mawasiliano na Walinzi wake Lakini Papy Kabamba akaondosha Hatari hiyo iliyotengenezwa na Mohammed Ibrahim.
Na dakika ya 85 Yanga wakajibu Mapigo Kwa kufanya shambulizi La kushtukiza Lakini Uimara wa Aishi Manula Uliwasaidia Simba kutokana na Shambulizi la Donald Ngoma.
Dakika ya 87 Yanga walifanya mabadiliko mengine kwa kumtoa Juma Abdul na Kumuingiza Hassan Hamis, Huku Erasto Nyoni akitolewa na Kuingia Mohammed Hussein wakati Kelvin Yondani akilishwa kadi ya Njano.
Penati za Kuamua.
Hadi Dakika 90 za Mwamuzi Heri Sassi zinamalizika Yanga SC hawakupata kitu wala Simba SC aliyepewa nafasi kubwa kushinda naye hakupata Kitu, ikilazimu mikwaju ya penati ipigwe Kuamua Bingwa.
Kelvin Yondani Ndio alikuwa wa kwanza kupiga penati na kipa Aishi Manula akapangua, Naye Method Mwanjali akafuata kwa upande wa Simba na Kukwamisha Mpira Wavuni.
Penati ya pili kwa Yanga ilipigwa na Papy Kabamba Tshishimbi ambaye alipiga penati Safi na kufunga, Huku Emmanuel Okwi akafuata kwa upande wa Simba na Kufunga.
Penati ya Tatu kwa upande wa Yanga Ilipigwa na Nahodha Thabani Kamusoko akafunga penati ya Ufundi, Naye Haruna Niyonzima akafuata kwa upande wa Yanga na kufunga.
Penati ya Nne kwa Yanga ilipigwa na Ibrahim Ajibu Migomba, ambaye Naye akamchambua Aish Manula na Kufunga, na upande wa Simba SC akaenda Kupiga Shizya Ramadhan Kichuya, na kumpeleka makalikiti kipa Youthe Rostand.
Donald Ngoma akaenda kupiga penati ya Tano kwa upande wa Yanga na kufunga, Huku Simba SC nao wakahitimisha kwa Mohamed Hussein kupiga penati iliyookolewa na Youthe Rostand.
Zikafuata penati moja moja, na Yanga wakaanza kwa Juma Mahadhi kupiga Juu na shuti lake kuota Mbawa, nafasi iliyotumiwa vizuri na Mohammed Ibrahim MO na kuwapa Ubingwa wa Ngao ya Hisani Simba SC baada ya kupata penati 5-4.
Huo unakuwa ubingwa wa Tatu kwa Simba SC kunyakuwa Ngao hiyo ambayo ni kiashiria cha Ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania Bara.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni