0
Mabingwa wa Azam Sports Federation Cup, Mnyama Simba Sports ClubJioni ya Leo wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mabingwa wa Ligi kuu Soka nchini Rwanda Rayon Sports.
Mchezo huo wa Kuadhimisha siku maalumu ya Klabu hiyo maarufu kama SIMBA DAY umefanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Simba ndio walioonekana bora zaidi toka dakika ya kwanza kwa kucheza soka la kasi na la kiufundi huku safu ya kiungo ikimilikiwa kikamilifu na Mghana James Kotei, Emmanuel Okwi, Mzamiru Yasini pamoja na Mohamed Ibrahimu.
Aidha Safu ya Ulinzi ya Simba SC ikiongozwa na Nahodha Method Mwanjali, Salum Mbonde, Erasto nyoni na Jamali Mwambeleko, ilikuwa Likizo kwa muda mrefu kutokana na wachezaji wa Rayon Sports kutofika sana katika Lango la Simba waliokuwa wakiadhimisha miaka 81 toka kuundwa kwa klabu yao.
Mohamed Ibrahim.
Bao la Simba katika Mchezo huo limefungwa na Mohamed Ibrahim 'MO' aliyefunga bao katika dakika ya 16 baada ya kupokea pasi maridadi kutoka kwa Mchezaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi na kuipitisha katikati ya mabeki wawili wa Rayon na kumshinda Mlinda Mlango Mutuyima Evariste.
Kiu ya Kumuona Kiungo mwenye thamani zaidi klabuni hapo, Haruna Niyonzima ambaye anakadiriwa kuwa na Thamani ya Zaidi ya shilingi Milioni 140, ilikatwa katika kipindi cha Pili baada ya Kocha Mkameruni Joseph Omog kumuingiza katika dakika ya 55.
Rayon Ilikuwa Pungufu.
Imeelezwa kwamba Rayon Sports wamekuja nchini kucheza na Simba wakiwa bila ya wachezaji wao mahiri Ndayishimiye Jean luc, Mutsinzi Ange, Manzi Thierry, Niyonzima Olivier, Sadaam na Muhire Kevin ambao wapo na Timu ya Taifa kujiandaa na mchezo wa kufuzu kwa Michuano ya CHAN dhidi ya Uganda.
Tuzo.
katika hatua nyingine Mchezo huo umeambatana na matukio mbalimbali likiwemo pambano la viongozi wa Klabu ya Simba na wafanyakazi wa Benki ya NMB, Lakini pia uagawaji wa Tuzo kwa Mchezaji Mohammed Hussein na Mkongwe Abdalah 'King' Kibadeni Mputa.
Mohamed Hussein alitwaa tuzo ya Mchezaji bora wa mashabiki wa Simba kwa Msimu uliopita wakati Mputa akitwaa tuzo ya Heshima ikiwemo kutambua mchango wake wa kuwa mchezaji pekee aliyefunga mabao matatu 'Hat Trick' katika mchezo dhidi ya Watani zao Dar young Africans

Chapisha Maoni

 
Top