0
Nguvu mpya Alexandre Lacazette alifunga magoli mawili na kuisaidia Arsenal kuicharaza Paris St-Germain 5-1 nchini Singapore.
Lacazette alifunga goli kutoka krosi ya Emile Smith-Rowe na kufunga bao jingine la kichwa likiwa la pili katika mchunao huo wa kirafiki.
Mesut Ozil , ambaye alistaafu kutoka soka ya kimataifa baada ya kombe la dunia , aliiongoza Arsenal kama nahodha na kufunga goili la kwanza , huku naye Rob Holding akifunga goli la nne kabla ya Eddie Nketiah kufunga udhia wa kukamilisha bao la tano.
Christopher Nkunku alikuwa ameisawazishia PSG baada ya kufunga penalti katika kipindi cha pili.
Penlati hiyo ilipigwa baada ya Sead Kolasinac kumuangusha mwanawe raia wa Liberia George Weah , Timothy katika eneo hatari lakini Arsenal ilizidisha nguvu na kufunga mabao manne zaidi.
Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery alikuwa amesema kuwa anataka manahodha watano katika kikosi chake msimu huu na kumpatia Ozil uongozi wa mechi hiyo.
Ozil alitaja ubaguzi na ukosefu wa heshima kuhusu mizizi yake ya Uturuki kuwa miongoni mwa sababu zilizomfanya kustaafu katika timu ya taifa ya Ujerumani lakini akaimarisha imani kwa mkufunzi wa wake kwa kufunga bao kufuatia pasi ya Emerick-Aubameyang
Ozil ni miongoni mwa wachezaji watano waliotolewa baada ya saa moja ya mchezo , na wachezaji wawili walioingia -mshambuiaji Lacazette na beki wa Uingereza Holding wote walifunga kabla ya Nketiah kuongeza bao la tano katika muda wa lala salama.



Kwamujibu wa 
BBC SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top