0
Kiungo wa Yanga, Pius Buswita amesema licha ya kufungwa na  Gor Mahia kwenye mchezo uliopita nchini Kenya wananafasi ya kuanza kupata pointi tatu kwenye mchezo wa marudiano kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga itakutana na Gor Mahia kwenye mchezo wao wanne kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwenye mchezo uliopita kwa mabao 4-0.
“Mpira kuna muda huwa na matokeo yasiyotarajiwa, tulipoteza kule, lakini safari hii tutakuwa nyumbani kwa hiyo ni matarajio yetu kupata ushindi kama maandalizi tumefanya ya kutosha,” alisema Buswita.
Nahodha wa Yanga, Juma Abdul alisema wachezaji wenzake wote wanamorali ya hali ya juu ili kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi.
"Kuanzia kambini mpaka mazoezi kila mchezaji yupo na hali na morali kuhakikisha tunashinda kwa mara ya kwanza tukiwa nyumbani," alisema Abdul.
Kama Yanga ikiibuka na ushindi katika mchezo huo kimahesabu itakuwa na nafasi ya kusonga mbele, endapo wakipoteza watasaliwa na michezo miwili dhidi ya Rayon na USM Alger ili wakamilishe ratiba.
Yanga inaburuza mkia katika msimamo wa Kundi D wakiwa na pointi 1 ambayo wameikusanya katika michezo mitatu, vinara wa kundi hilo ni USM Alger ambao wanaongoza wakiwa na pointi saba na wanaofuata ni Gor Mahia wenye pointi tano.



Kwamujibu wa 
Mwanasport

Chapisha Maoni

 
Top