Mshambuliaji wa kimataifa Tanzania, Saimon Msuva anahitaji bao moja kuivunja rekodi ya Mbwana Samatta aliyoweka 2012 akiwa na TP Mazembe katika mwaka wake wa kwanza.
Samatta katika msimu wake wa kwanza baada ya kujiunga na TP Mazembe akitokea Simba aliisaidia timu hiyo ya DR Congo kucheza nusu fainali baada ya kufunga mabao sita katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Jana Ijumaa mshambuliaji wa zamani ya Yanga na Diffa El Jadida, Msuva amefunga bao lake la tano katika Ligi ya Mabingwa katika msimu wake wa kwanza na miamba hiyo ya Morocco.
Mabao hayo yanamfanya Msuva kuwa nafasi ya tatu katika orodha wafungaji akiongoza mshambuliaji mwenzake wa Difaa el Jadida, Ahaddad mwenye mabao saba.
Msuva alifunga bao hilo dakika 23, kabla ya ES Setif kusawazisha kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na EL Habib Bouguelmouna katika dakika 32, Diffa El Jadidi ililazimisha sare 1-1 na ES Setif kwenye Uwanja wa El Abdi.
Matokeo hayo yanaifanya Difaa kuendelea kubaki mkiani mwa kundi hilo linaloongozwa na TP Mazembe ikifuatiwa na Setif, MC Alger ni ya tatu.
Wakati Difaa ikichechemea Msuva kwake binafsi mambo safi akiweka rekodi ya kufunga mabao matano kwa mara ya kwanza akiwa na klabu hiyo ya Morocco.
Orodha ya wafungaji
Mabao 7) Ahaddad (Difaa el Jadida)
6) Badri (Esperance/TUN), Malango (TP Mazembe/COD), Nekkache (Mouloudia Alger/ALG)
5) Msuva (El Jadida), Haddad (Wydad Casablanca/MAR)
4: Adams (Zesco Utd/ZAM), Badenhorst (Mbabane Swallows/SWZ), Mundele (V Club/COD)
Kwamujibu wa
Mwanasprt
Chapisha Maoni