0
MSHAMBULIAJI wa Levante UD, Roger Marti amemkaribisha nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kwenye klabu hiyo itakayoshiriki msimu ujao wa  Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ huku akiwa na uhakika kukutana na Lionel Messi.
Roger mwenye uraia wa Hispania, amedai kuzisikia taarifa za Samatta kuwaniwa na klabu hiyo ambayo imelenga kuboresha safu yake ya ushambuliaji.
Siku chache zilizopita vyombo vya habari vya Hispania  viliripoti kuwa Levante wameingia msituni kwa dau la Sh 10.6bilioni kwa ajili ya kuinasa saini ya Samatta ili azibe pengo la Mghana Emmanuel Boateng aliyepata majeraha.
Mshambuliaji Roger ameiambia tovuti ya Mwanaspoti atakuwa tayari kutoa ushirikiano kwa Samatta ili azoee kwa haraka aina yao ya uchezaji na mazingira kwa ujumla.
“Nasikia ni mchezaji mzuri ambaye amewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ndani kwa wachezaji wa Afrika, nadhani atafurahia maisha yake mapya hapa kama atajumuika nasi,” alisema Roger.
Kufuatiwa kuumia kwa Boateng, Levante ambayo msimu uliopita walimaliza kwenye nafasi ya 15 wakiwa na pointi 46 wamesaliwa na washambuliaji wa tatu akiwemo Roger.
Washambuliaji wengine ni Mualbania Armando Sadiku na Mhispania David Salgueiro ambao wameshindwa kuwania namba ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi hicho mbele ya Boateng.
Samatta ambaye pia anawaniwa na CSKA Moscow ya Russia alifunga mabao 21 kwenye msimu wake wa kwanza Ubelgiji akiwa na klabu yake ya KRC Genk.
Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Samatta kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti, Boateng ambaye alikuwa akitegemea na Levante alifunga mabao sita.
Kinara wa mabao kwa Levante msimu uliopita alikuwa ni kiungo José Luis Morales aliyefunga mabao 10 huku pia akitengeneza nafasi nane za mabao.


Kwamujibu wa 
Mwanasport

Chapisha Maoni

 
Top