0
Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF
limeteua Watanzania kuwa maofisa
waandamizi watatu kusimamia
mchezo wa kundi A kati ya Ghana na
Gabon wa michuano ya Afrika chini ya
umri wa Miaka 17 utakaofanyika
Katika Uwanja wa Port Gentil,
Jumatano.
Watanzania hao ni Mwesigwa Joas
Selestine atakayekuwa Kamisha wa
mchezo huo, wakati Frank John
Komba atakuwa mwamuzi msaidizi na
katika kitengo cha kitaalamu cha
uchunguzi kwa wachezaji wanaotumia
dawa za kusisimua misuli atakuwako,
Dk. Paul Gasper Marealle.
Ni Sifa.
Uteuzi huo umepokelewa kwa furaha
na Shirikisho la Soka nchini TFF na
kusema kuwa Hiyo ni fahari kwa nchi
kwa viongozi wake kuthaminiwa na
kuaminika katika nyanja za kimataifa.
Aidha TFF imewapongeza na
imewatakia kila la kheri katika
kutimiza majukumu waliyopangiwa na
hasa ikizingatiwa kuwa fainali zijazo
za vijana kama hizi, zitafanyika
Tanzania mwaka 2019.

Chapisha Maoni

 
Top