unatarajiwa kukutana na
mfanyabiashara Mohammed
‘Mo’ Dewji katika kikao
maalum cha kumaliza tofauti
zilizojitokeza baada ya klabu
kuingia mkataba wa
udhamini na kampuni ya
SportPesa.
Na hiyo inafuatia kikao cha
suluhu juzi kuamkia jana
baina ya Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya Simba,
Zacharia Hans Poppe na
Kamati ya Utendaji ya klabu
chini ya Rais, Evans Elieza
Aveva.
Hans Poppe alijiuzulu
Ujumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Simba juzi na
maana yake kujivua pia na
uongozi wa Kamati ya Usajili
na ya ujenzi wa Bunju
Complex baada ya
kuchukizwa na kutohusishwa
katika mkataba wa udhamini
wa kampuni ya SportPesa.
“Siyo kushirikishwa mimi tu,
bali Wajumbe wengine wa
Kamati ya Utendaji pia, lakini
kubwa zaidi tuna
makubaliano na Mo (Dewji)
kuwa tukitaka kuingia
mkataba na yeyote yule,
hakatai lakini tumshirikishe,
sasa tunasaini mkataba kwa
kumzunguka ni kukosa
uungwana na siwezi kuwa
sehemu ya hilo,”alisema
akizungumza juu ya
kujiuzulu kwake.
Poppe alisema kwamba
alijaribu sana kutaka
kukutana na viongozi wa
Simba kujadili nao suala hilo,
lakini walikuwa wanamkwepa
ndiyo maana akaamua
kujiuzulu; “Hatujakaa, kila
nikiwaambia tulijadili
wanaingilia huku wanatokea
kule,” alisema juzi usiku.
Lakini jana Poppe alisema
kufuatia kikao chake na
uongozi wa Simba juzi usiku
wamemaliza tofuti hizo na
kufikia makubaliano ya
kurudi kuzungumza na Mo
Dewji wamalize utata uliopo.
Dewji anayetaka kununua
hisa Simba, alikasirishwa na
uongozi wa klabu hiyo kwa
kuingia mkataba wa
udhamini na kampuni ya
SportPesa bila
kumshirikisha.na akataka
alipwe fedha zake, Sh Bilioni
1.4 alizokuwa anaikopesha
Simba kwa kulipa mishahara
ya wachezaji na benchi la
Ufundi, Sh Milioni 80 kila
mwezi.
Ikumbukwe Mo alikubaliana
na uongozi wa Simba
kununua asilimia 51 ya hisa
kwa Sh. Bilioni 20 mara
baada ya mchakato wa
mabadiliko ya Katiba
utakapokamilika. Na katika
makubaliano ya msingi baina
yake na uongozi ni kwamba
ikitokea kampuni inataka
kuidhamini klabu
ashirikishwe, jambo ambalo
halikufanyika.

Chapisha Maoni