0
Mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard yuko katika mazungumzo ya mwisho ya kuongeza mkataba na klabu hiyo.

Kama watakubaliana Hazard atakuwa ndiye atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi kuliko wengine wote Chelsea kwa kuwa anatarajia kuanza kupata
pauni 200,000 kwa wiki.

Taarifa zimeeleza kupitia mwanasheria wake, Hazard yuko katika hatua za mwisho za makubaliano ya kusaini mkataba huo mpya.

Iwapo watakubaliana, mkataba utakuwa wa miaka mitano na Hazard atabeba pauni milioni 10.
Mbelgiji huyo ni kati ya wachezaji nyota zaidi Chelsea na katika Ligi Kuu England. Timu kadhaa kama Barcelona, Real Madrid, AC Milan zimekuwa
zikimtolea ‘mimacho’,

Chapisha Maoni

 
Top