wamepinga vikali kitendo cha baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kumshambulia kwa maneno ya kejeli aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba wakidai mashambulizi hayo yaelekezwe kwa wananchi waliotoa maoni yao katika tume.
Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti mjini humo jana, wakazi hao wamedai kauli na matusi
yanayotolewa na baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo ni utovu wa nidhamu uliovuka mipaka.
Walidai kushangazwa na shutuma, kejeli, matusi na lawama ambazo zinaelekezwa kwa Jaji Warioba wakidai kilichofanywa na tume yake ni
kukusanya maoni ya wananchi, kuchambua mambo ya msingi na kuyaweka kwenye Rasimu
ya Pili ya Mabadiliko ya Katiba.
Kwa upande wake, Maige Mbogo, mkazi wa Kata ya Mwasele, Manispaa ya Shinyanga, alisema kama wajumbe wa Bunge hilo hawayaamini maoni
yaliyokusanywa na tume ni vyema wakaenda kwa wananchi kuwauliza upya.
“Hakuna sababu za kumtukana Jaji Warioba, waje kutuuliza juu ya maoni yaliyopo kwenye rasimu nasi tutawapa ukweli kwamba yaliyoandikwa
kwenye rasimu ndio maoni yetu, kimsingi tunataka mabadiliko katika nchi yetu,” alisema. Kwa upande wake, Katibu Mwenezi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Shinyanga Mjini, Charles Shigino, naye alidai kushangazwa na kauli za kumshambulia Jaji Warioba akidai zinaweza kuwa
na athari kubwa ndani ya chama wakati wa chaguzi zijazo nchini.
Mkazi wa Kata ya Masekelo, Juma Shabani, alimshangaa mbunge wa Mbinga Kusini, Bw. John Komba (CCM), kwa kumtuhumu Jaji Warioba
akidai anawachanganya wajumbe wa Bunge hilo.
Credit: Majira
Chapisha Maoni