0
ARSENAL imetoka nyuma na kushinda 2-1 katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya ugenini usiku huu.
Shukrani kwake, Lukas Podolski aliyetokea benchi ambaye alifunga bao la ushindi dakika ya 91 mjini Brussels, Ubelgiji baada ya The Gunners kutanguliwa kutunguliwa kwa bao la
Andy Najar dakika ya 72.

Lakini Kieran Gibbs aliisawazishia timu ya Arsene Wenger dakika ya 88 kabla ya
Podolski kuleta ushindi. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Borussia Dortmund imeichapa 4-0 Galatasaray nchini Uturuki.

Kikosi cha Anderlecht kilikuwa: Proto, Vanden Borre, Mbemba, Deschacht, Acheampong, Tielemans, Defour, Najar, Praet/Dendoncker dk88, Conte na Cyriac/Suarez dk83.

Arsenal: Martinez, Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Flamini/Oxlade-Chamberlain dk74, Sanchez, Ramsey, Wilshere/Podolski
dk84, Cazorla na Welbeck/Campbell

Chapisha Maoni

 
Top