REAL Madrid imeichapa mabao 3-0 Liverpool Uwanja wa Anfield, katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo aliwafungia Real bao la kwanza dakika ya 23, kabla ya Karim Benzema kufunga la pili dakika ya 30 na la tatu dakika 11 baadaye.
Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli
alibadilishana jezi na beki Pepe wakati wa mapumziko kabla ya kumpisha Adam Lallana. Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, PFC Ludogorets Razgrad imeichapa bao 1-0 FC Basel.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet,
Johnson, Skrtel, Lovren, Moreno, Henderson/ Can dk67, Gerrard, Allen, Sterling, Balotelli/ Lallana dk45 na Coutinho/Markovic dk67.
Real Madrid: Casillas, Arbeloa, Varane, Pepe, Marcelo/Nacho dk85, Modric, Kroo/ Illarramendi dk82, Rodriguez, Isco, Benzema na Ronaldo/Khedira dk75, 6.
Chapisha Maoni