ATLETICO Madrid imeendeleza moto wake katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuichapa mabao 5-0 nyumbani Malmo FF ya Sweden katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ushindi huo umetokana na mabao ya Koke dakika ya 48, Mandzukic dakika ya 61, Griezmann dakika ya 63, Godin dakika ya 87 na Cerci dakika ya 90 na ushei. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Olympiacos imeshinda 1-0 nyumbani dhidi ya Juventus. Katika mechi za Kundi C, Bayer Leverkusen
imeshinda nyumbani mabao 2-0 dhidi ya Zenit St Petersburg wakati Monaco
imelazimishwa sare ya 0-0 nyumbani na
Benfica.
Chapisha Maoni