0
KLABU ya Liverpool imeichapa Swansea
mabao 2-1 katika mchezo wa Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Capital One Cup usiku huu Uwanja wa Anfield.

Jordan Henderson alipewa beji ya Unahodha, kocha Brendan Rodgers akifanya mabadiliko ya wachezaji tisa katika kikosi chake chavkwanza.

Winga wa Swans, Marvin Emnes aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya 65, kabla ya Mario Balotelli aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Rickie Lambert kusawazisha zikiwa
zimesalia dakika tano.

Federico Fernandez alitolewa kwa kadi
nyekundu dakika za mwisho kwa kumchezea rafu Philippe Coutinho kabla ya Dejan Lovren kuifungia Liverpool bao la ushindi dakika za majeruhi na kuwapeleka Wekundu hao Robo
Fainali.

Chapisha Maoni

 
Top