KLABU ya Chelsea imetinga Robo Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup baada ya kuichapa mabao 2-1
Shrewsbury usiku huu. Chelsea ilipata bao la kwanza mapema tubkipindi wakati mkongwe, Didier Drogba
alipomalizia pasi maridadi ya mwanasoka wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah.
Lakini Shrewsbury ikapata bao la
kusawazisha kupitia kwa Andrew Mangan aliyetokea benchi dakika ya 77, kabla ya Jermaine Grandison kujifunga dakika nne baadaye kuipa ushindi timu ya Jose Mourinho.
Chapisha Maoni