KIPA wa Rangers, Steve Simonsen alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kujigonga kwenye nguzo ya lango huko Ibrox jana.
Timu ya Ally McCoist ilikuwa mwenyeji wa timu ya Ligi Kuu, St Johnstone katika Robo Fainali ya Kombe la Ligi Scotland wakati Simonsen alipojiumiza mwenyewe katika harakati za kuokoa.
Mlinda mango huyo mwenye umri wa miaka 35 nafasi yake ilichukuliwa na Lee Robinson baada ya kutolewa uwanjani akiwa amebebwa kwenye machela mwanzoni mwa kipindi cha pili, kabla ya bao la kichwa la Lewis Macleod dakika nne kabla ya filimbi ya mwisho
kuamua mshindi.
Kocha wa Rangers, Ally McCoist alisema
baada ya ushindi huo kwamba Simonsen anapatiwa matibabu hospitali baada ya kuumia akiokoa mchomo wa kichwa wa Brian Graham kipindi cha pili.
Chapisha Maoni