mkoani Dodoma imesema
haitawavumilia walimu walevi, pia
walimu wa kike wanaovaa mavazi
mafupi na yanayoonesha maungo ya miili
yao na walimu wa kiume wanaovaa
suruali za kubana ‘vimodo’. Kauli hiyo
ilitolewa juzi na Ofisa Elimu wa Wilaya
ya Bahi, Mary Mathew wakati
akizungumza na walimu wapya wa shule
za msingi kwenye semina elekezi
inayohusu utendaji wa kazi zao.
Alisema ualimu ni kazi inayohitaji
nidhamu ya hali ya juu kutokana na
walimu kuwa walezi wa watoto
wanaokuwa wanawafundisha, kwa hiyo
ni vyema wakavaa mavazi ya heshima
kutokana na wao kuwa kioo cha jamii.
Alisema ni marufuku kwa walimu kuvaa
nguo fupi na zile zinazoonesha maungo
ya miili yao.
“Walimu watakiwa kuonesha maadili
mema kwani ni mabalozi kwa jamii
inayowazunguka pamoja na wanafunzi
wanaowafundisha,” alisema .
Alisema hatarajii kuona walimu wanavaa
nguo zinazodhalilisha taaluma hata kama
wao wanazipenda.
“Hasa ninyi kinadada na hata vijana
mkinivalia vimodo, kwa kweli
sitowavumilia walimu ndani ya Wilaya
hii ya Bahi kwani mnatakiwa kuonyesha
mfano kwa jamii na wanafunzi
mnaowafundisha,’’ alisema.
Pia aliwataka walimu hao kuzingatia
miiko ya kazi kwa mujibu wa waraka na
sheria za serikali, ili kuleta ufanisi katika
kuboresha elimu.
Alisema walimu wengi wanapopata ajira
wamekuwa wakijisahau kama wao ni
watumishi wa Serikali na kufanya
maamuzi ambayo ni kinyume na waraka
na maagizo ya kazi zao.
Naye, Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Bahi
Fredrick Kayombo amewashauri walimu
hao kutumia fursa zao katika kuanzisha
miradi itakayowafanya wakopesheke
kwenye taasisi za kifedha.
Pia aliwataka hao wanapokuwa kwenye
vituo vyao vya kazi kujihadhari na
matumizi ya muda wa kazi pindi
wanapokuwa kazini.
“Kamwe hatutawavumilia walimu
watakaobainika kutumia muda huo wa
kazi kwa unywaji wa pombe,” alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Bahi, Rachel Chuwa
alisema wilaya hiyo imepata walimu
wapya zaidi ya 70 na utaratibu wa
mafunzo elezi kwa walimu wapya una
lengo la kuwaondolea woga na hofu
walimu ili waweze kufanya kazi zao
vizuri.
Alisema mwaka jana wilaya hiyo ilishika
nafasi ya tano kati ya saba kwa ufaulu
mkoani Dodoma na anatumaini walimu
hao watasaidia kuongeza kiwango cha
ufaulu kutokana na kuonesha ari ya
kufanya kazi.
“Nitasikia amani kubwa kama
mtaipandisha Bahi na kuwa nafasi ya
juu,” alisema.
Pia aliwataka walimu hao kutulia kwenye
vituo vyao vya kazi kutokana na baadhi
ya walimu kuanza kuomba uhamisho
kwa kisingizio cha ndoa.
“Kila kitu kina utaratibu wake kumbuka
umeshaingia kwenye ndoa na Serikali
kwenye hilo tutaangalia ya kisheria na
yale ya kimahusiano hata masuala ya
ugonjwa yataangaliwa lazima tuheshimu
sheria, kanuni na utaratibu wa kufanya
kazi,” alisema.
Chapisha Maoni