0
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wenzake 8 leo wamepata dhamana katika Mahakama ya Kisutu,
Dar. Kesi yao kutajwa tena Oktoba 21, 2014.
Siku ya jana washtakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Kaluyenda na kusomewa
mashtaka mawili na Wakili wa Serikali Mkuu, Kangola aliwataja washtakiwa kuwa ni Mbunge wa Kawe, Mdee, Rose Moshi, Penina Peter, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fanuel, Edward
Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari.

Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa Ufipa
wilayani Kinondoni, walikaidi amri ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf iliyowataka watawanyike.
Shtaka la pili washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba
4, mwaka huu, maeneo ya mtaa wa ufipa jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo moja walikusanyika
kinyume na sheria wakitaka kwenda ofisi ya rais.

Chapisha Maoni

 
Top